MOURINHO APEWA DILI MAN UNITED VS LIVERPOOL.
Saturday octoba 19 2019
Na mwandishi Christer Shechambo
Jose MOURINHO anatarajiwa kuwa mchambuzi wa michezo kesho jumapili kati ya Manchester United dhidi ya Liverpool.
Jose MOURINHO anatarajiwa kuwa mchambuzi wa michezo kesho jumapili kati ya Manchester United dhidi ya Liverpool.
Uamuzi you umechukuliwa na kituo cha runinga cha sky sports ambapo baadhi ya mashabiki wa Manchester United wameshangazwa nakuamin itakuwa ni nafasi ya kocha huyo kuendelea kuiponda united.
Mchezo kama you ndio ambao ulisababisha united kumfukuza kazi mourinho, decemba mwaka jana baada ya liverpool kushinda bao 3-1.timu hizo zinakutana huku kukiwa na presha kubwa kwa kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer kutokana na matokeo mabaya ya simu huu.
Inaaminika kuwa historia inaweza kujirudia kwa solskjaer kupoteza kazi kama ilivyokuwa kwa mourinho ikiwa timu yake itapata kipigo likali kutoka kwa wapinzani wao wa jadi.
Kocha wa liverpool Jurgen Klopp anatarajiwa kuingiza kikosi kikiwa na nguvu kwa kuwa timu yake imekuwa ikifanya vizuri tangu kuanza kwa msimu huu licha ya kuwa mchezo utapigwa kwenye uwanja wa old Trafford ambapo ni ugenini kwao.
Washabiki wengi mtandaoni wametoa maoni ya kushazwa na uamuzi huo wa sky kumpa nafasi mourinho kuchambua mchezo huo huku wale wapinzani wa United wakifurahia kwa kuwa na hamu ya kusikia atakachozungumza.



0 Comments