LIVERPOOL  KICHEKO MANCHESTER UNITED TIA MAJI -TIA MAJI 
Na mwandishi christer shechambo 

London-England ni mwaka wa tabu ndicho unachoweza kusema kuwa manchester United.wakati kikosi chao kamili kinaonekana kitakuwa vibonde kwa liverpool jumapili bado wameendelea kukumbana na majanga baada ya kutupa nambari moja David De Gea kuumia juzi.

De Gea ambaye ni mmoja kati ya makipa mahiri duniani aliumia katika pambano la kufuzu michuano ya Europe 2020 kati ya taifa lake Hispania dhidi ya Sweden lililochezwa jijini Stock holm Juzi likamalizika Kwa sare Ya 1-1.

De Gea alionekana kuumia na kuchukizwa katika dakika ya 60 baada ya kuosha mpira lakini akakaa chini na kulalamikia nyonga yake akiwa katika maumivu. Wakati huo Sweeden walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0 katika pambano hilo la kundi kufuatia bao safi la Marcus Berg katika dakika ya 50.

De Gea alishindwa kuendelea na kutolewa nje na madaktari wa Hispania huku nafasi yake kuchukuliwa na kipa namba moja wa Chelsea kipa Arrizabalaga ambaye katika miezi ya karibuni amekuwa chaguo la kwanza Hispania lakini aliachwa nje katika pambano la juzi baada ya kufanya kosa la kizembe katika pambano dhidi ya Norway jumamosi usiku.