siku chache zilizopita msanii wa muziki wa bongo flava vanessa mdee v-money alithibitisha kuwa na penzi jipya na staa wa hollywood ,marekani mwenye asili ya Nigeria ,Rotimi,jamaa huyo amekuwa akipondwa kinoma mtandaoni ,kiasi cha kumfanya mwanamama zarinah hassan "zari the bosslady"kumkingia kifua.
Baadhi ya watu wa mitandaoni hasa instagram waliponda kapo hiyo huku wakidai Rotimi ana pua kubwa,jambo lililomfanya zari ambaye ni" eski" wa diamond kujitosa kumtetea.
katika moja ya posti za kumponda jamaa huyo kwenye instagram ,zari aliandika; 'ndiyo maana wanaume tunawaficha siku hizi kwa sababu mashemeji wa instagram hawajatulia kabisa ,hakuna mtu sahihi hivyo mwacheni vee (vanessa)."
0 Comments