WAFANYA KAZI 127 WAPOTEZA AJIRA
Na christer shechambo
Na christer shechambo
Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwamo kutoka Tanzania, wapo hatarini kupoteza ajira zao kutokana na mageuzi makubwa yanayofanywa
IMawaziri wanaohusika na jumuiya hiyo tayari wamepitisha mpango wa kufanyika mageuzi katika taasisi hiyo utakaowezesha nchi sita wanachama kuokoa Dola za Marekani milioni 2.5 kwa mwaka kutokana na mishahara ya wafanyakazi.
Ikiwa mpango huo utatekelezwa, nafasi za ajira ndani ya EAC zitapungua kutoka 529 mpaka 402 katika vitengo vyote na taasisi zake.
Mageuzi hayo yamepitishwa wakati wa mkutano wa 30 wa mawaziri wa mambo ya EAC na mipango (SCMEACP), uliofanyika makao makuu ya jumuiya hiyo jijini Arusha Mkutano huo uliofanyika chini ya mwenyekiti wake, Waziri anayeshughulikia EAC kutoka Rwanda, Balozi Olivier Nduhungirehe, ulijadili ripoti ya dharura katika muundo wa kazi na ajira katika taasisi hiyo.
EAC kwa miaka mingi imekuwa ikikabiliana na changamoto mbalimbali ikiwamo suala la ajira kutokana na ukosefu wa sera ya uwiano wa ajira baina ya nchi wanachana na kusababisha migogoro.
“Mageuzi ya taasisi katika jumuiya yaliyofanyika yamekuwa katika mchakato kwa takribani muongo mmoja sasa na Jumamosi iliyopita tumekubaliana kufanya mageuzi katika muundo wa taasisi za jumuiya,” alisema Nduhungirehe alipokuwa akizungumza na gazeti la The New Times la nchini Rwanda.
Maamuzi ya mawaziri wa EAC yametokana na mkutano wa EAC uliofanyika Kampala, Uganda mwaka jana, ambapo viongozi wa ukanda huo waliomba idadi ya manaibu makatibu wakuu kupunguzwa kutoka wanne mpaka wawili Nduhungirehe alisema kwa sasa kuna manaibu wawili ambao wanashirikiana katika majukumu yao katika kukuza ushirikiano EAC, mmoja akishughulikia masuala ya ushuru wa pamoja na soko la pamoja na mwingine masuala ya sarafu ya pamoja na shirikisho la kisiasa.
“Hatuna mkurugenzi mkuu katika biashara na forodha, lakini tuna mkurugenzi mkuu wa huduma za ushirikiano,” alisema.
Nduhungirehe alieleza kuwa wameelekeza tume ya huduma za EAC kuwasilisha mpango wa kutekeleza maamuzi hayo katika mkutano ujao wa baraza la mawaziri uliopangwa kufanyika mwishoni mwa Novemba.
Imeelezwa kuwa, kazi ya uchambuzi wa nafasi za ajira umefanywa na wataalamu kutoka nchi sita wanachama kuanzia Machi mwaka jana kwa lengo la kuanzisha muundo mpya wa ushirikiano utakaoruhusu ufanyaji maamuzi kwa kasi kwa kutumia rasilimali chache.
Mmoja wa wabunge wa EAC kutoka Tanzania ambaye hakutaka kutajwa jina lake, amekiri kuwapo kwa mpango huo na kulieleza gazeti hili kwamba, suala hilo bado lipo katika ngazi ya baraza la mawaziri.
Alisema baada ya kupitishwa kwa maamuzi hayo, yatapelekwa katika kamati ya bajeti kisha katika Bunge la jumuiya hiyo.
Alisema katika kikao hicho, Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Damas Ndumbaro, ambaye alipotafutwa na gazeti hili jana ili kuthibitisha simu yake haikupatikana hewani.
Mbunge mwingine wa jumuiya hiyo kutoka Tanzania, Habib Mnyaa, alisema suala hilo litakapofika katika ngazi yao ya wabunge watapata nafasi ya kutoa mtaasisi hiyo, lakini katika masuala ya kisiasa hakutakuwa na tatizo tofauti na maeneo mengine ya kitaaluma.

COPY SUCCESS




0 Comments