Na Bosco Kayombo
Yule fundi wa mpira, mkali wa kupiga pasi mnyaruwanda,Haruna Bizimana Niyonzima ,bado yumo katika midomo ya mashabiki kwa soka Tanzania, hususan baada ya kufanya mambo makubwa akizichezea timu kongwe za simba na yanga kwa nyakati tofauti.

Kiungo huyo ambaye kwa sasa amerejea nchini kwao, juzi alikuwa sehemu ya kikosi kilichoanza cha timu ya taifa Rwanda kilichoana nataifa stars katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa ardhi ya kwao kigali.
Baada ya kukutana na wachezaji kadhaa alikipiga nao alipokuwa nchini Tanzania, habari nyepesi nyepesi kwamba anafikiria kurudi yanga ,DIMBA jumatano litajiongeza kupata ukweli .
Niyonzima mwenyewe alikiri kwamba mchezo wa soka ndiyo maisha yake na unaweza kumrudisha Tanzania endapo mipango hiyo itaruhusu kufanya hivyo.
Lakin makamu mwenyekiti wa yanga,Fedrick Mwakalebela yeye ndiye aliyefunguka zaidi kuhusu taarifa zinazoenea juu ya kurejea kwa kiungo was huyo wa zamani,ambaye sasa anakipiga katika kikosi cha AS Kigali.

0 Comments