Magufuli ampa Mbalawa siku 7
Rais
John Magufuli amesema ameanza ziara yake mkoani rukwa vibaya na kwa majonzi
kutokan na ujenzi wa miradi ya maji yenye thamani ya Sh bilioni 20 kutekelezwa
na mkandarasi Fally Enterprises asiye na sifa wala uwezo ambaye ameagiza
achunguzwe na kushitakiwa.
Kutokana
na hali hiyo amemuagiza Waziri wa maji, Profesa Makame Mbalawa kuchukuliwa
hatua kali watendaji wa wizara yake waliohusika kumpatia kazi nyingi zaidi
mkandarasi huyo kinyume cha taratibu.
Aidha
amemuagiza Profesa Mbalawa na kumpatia siku saba kuunda tume maalumu ya
uchunguzi wa kina miradi yote inayotekelezwa na mkandarasi huyo ikiwemo ile
ambayo haijakamilishwa.
Mbali ya
wizra ya maji pia ameagiza Tamisemi,
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, mkoa wa Rukwa, kamanda wa Polisi wa Mkoa,
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa na Wakili wa Serikali
kufuatilia tuhuma dhidi ya mkandarasi huyo pamoja na hujuma uliofanywa katika Mradi
wa maji Laela.
Pia
amempigia simu na kumuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, (IGP) Simon Siro
kumuondoa Ofisa Mnadhimu, Polycarp Urio kwa kushindwa kutekelezwa kwa agizo la
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiwa ziarani Rukwa hivi
karibuni.\
Rais
Magufuli ametoa maagizo hayo jana katika mji mdogo wa Laela Halimashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
kabla ya kuzindua barabara ya Tunduma-Laela-Sumbawanga kilometa 223.2
iliyogharimu Sh bilioni 375.
Mradi
huo wa barabara ulikamilika kujengwa tangu mwaka 2015 kwa ufadhili wa serikali
ya Marekani kupitia shirika lake la Millennium Challenge (MCC) na fedha za
ndani za serikali ya Tanzania kwa kiwango cha lami.
“Huyu
mkandarasi Fally hamalizi ujenzi wa miradi huku mingine ikiwa chini ya kiwango,
nashangaa amepewa miradi yote.. lakini hajafutiwa usajili kwa mujibu ya sheria
namba 15 ya 1994” alieleza Rais Magufuli.
“Waziri
andaa wizara maalumu ichunguze miradi yote ya maji anayoijenga pia ifanyiwe
upya tathimini pamoja nakubaini kama utaratibu wa manunuzi umefuatwa kwa mujibu
wa sheria. Kama mkandarasi huyo amelipwa waziri baada ya kuwasilisha
Certificate zote mlipaji awekwe ndani kwa mjibu wa sheria” alizidi kuagiza Rais
Magufuli.
Alimwagiza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Selemani Jafo kumfuatilia Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Nyangi Msemakweli kama amemlipa
mkandarasi huyo.
Mkandarasi
huyo anatuhumiwa kuhujumu miradi ya maji kwa kuijenga kwa viwango hafifu ukiwemo
mradi wa maji wa Laela wa gharama ya zaidi ya Sh bilioni 1.7 ukiwa umemalizika
miaka mitatu iliyopita lakini maji hayatoki.
Miradi
iko katika Katika Wilaya za Kalambo Nkasi na Sumbawanga.
“Ninazo
taarifa kuwa Profesa Mbalawa ulipokuwa Mkoani Rukwa kikazi aliagiza mkandarasi
Fally akamatwe lakini akaachiwa. Nataka nimfahamu nani aliyemuachia huru
akikaidi agizo la Waziri ambaye ni mteule wangu” amehoji huku akiwataka
viongozi wasitishwe na watu wenye fedha.
Awali, Mbunge wa Nkasi Kasikazini, Ally Kessy
alimweleza Rais Magufuli kuwa mkandarasi Fally hana sifa na viwango, na
amefisadi miradi ya maji huku akijilimbikizia mali kwa kujenga maghorofa sehemu
mbalimbali.
“Mheshimiwa
Rais mafisadi kama Fally wanastahiki adhabu kali ya kunyongwa pia azitapike
fedha zote kama wengine wanavyozitapika” alisema mbunge huyo machachari.
Baada ya
kuzindua barabara, Rais alifika kituo cha polisi wilaya ya kipolisi ya Laela na
kumpgia IGP Sirro na kumuagiza amfukuze mnadhimu Urio kwa kushindwa kumpatia
RPC majina tisa ya asikari polisi ambapo waziri Lugola aliagiza wahamishwe kwa
makosa ya kuwabambikizia kesi wananchi na kuwanyima dhamana.
Rais
Magufuli ambaye alitokea mkoani Songwe alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku
tatu, jana alianza ziara mkoani Rukwa ambayo inaendelea leo. Akimaliza mkoani
humo atakwenda kwa ziara nyingine mkoa wa Katavi.
MWISHOO….


0 Comments