Na Winston kinyaha
Ni Mfalme aliyejipatia umaarufu Barani Afrika na duniani kwa ujumla hasa kutokana na utamaduni wake wa kuoa wake wengi.
Mfalme huyo wa taifa la zamani la Swaziland ambalo alilibadilisha jina
kulibatiza jina jipya la Ufalme wa eSwatini. Alitoa tamko hilo mwaka
jana 2018 wakati wa maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa alipokuwa
akitimiza miaka 50 ya kuzaliwa.
eSwatini, lina maana ya ardhi ya Waswaz na lilitumiwa rasmi na Mfalme Mswati wa tatu kwa miaka mingi. .
Mfalme huyu amejitwalia umaarufu kwa kuoa wake wake 15, ambapo wake zake
wawili waliamua kumwacha na wawili wengine walifariki dunia, kwa sasa
King Mswati III anadaiwa kuwa na watoto 34 na wajukuu 4.
Katika mila na desturi za Swaziland (eSwatini) Mfalme anahitajika
kuchagua miongoni mwa halaiki ya wasichana ‘vipusa’ walio bikra kila
mwaka katika ngoma maarufu ya ‘Reed Dance’ inayoitwa Umhlanga. .
Taifa hilo ni mmoja kati ya nchi 16 zilizohudhuria mkutano wa 39 wa
wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)
uliofanyika jijini Dar es Salaam.


0 Comments